karibu kituo cha nishati

KITUO CHA NISHATI MBADALA KATA YA OLDONYOSAMBU:karibu kupata huduma ya nishati mbadala kituoni,mifumo ya paneli za umeme jua; saizi tofauti tofauti:-SOLATA inayochaji simu,TOCHI inayochaji betri. MGAHAWA KUTUMIA MAJIKO SANIFU,HUDUMA ZA COMPUTER,MAJIKO SANIFU NA BANIFU:-jiko janja,kapu la ajabu,MITI MICHE YA AINA MBALIMBALI INAPATIKANA:-parachichi, mibono,albizia, groton,moringa, markhmla, na mingineyo. MITAMBO YA GESI, SABUNI ZA MBONO JATROPHA, na USHAURI KEM KEM WA KUTOKA KWA MAMA NISHATI.

Thursday, February 24, 2011

KWANINI NITUMIE MFUMO WA PANELI ZA UMEMEJUA?

FAIDA:
1. Unatoa mwanga wa kutosha kunapokuwa na giza;
2. Huepusha magonjwa ya kupumua yanayosabishwa na taa zinazotumia mafuta ya taa ;
3. Unatoa fursa ya kuchaji simu na kusikiliza redio;
4. Ni teknolojia ya uhakika ;
5. Unahitaji ukarabati mdogo na rahisi;
6. Unaweza kuubadilisha kwa kuongeza paneli au betri baadae.

HASARA:


1. Gharama za awali ni kubwa lakini hulipa kwa kuzingatia fursa ya kulinda afya na kuokoa pesa baada ya muda kama mwaka mmoja;
2. Mfumo unahitaji kugharamia kirekibishi kwa vifaa vinavyotumia umeme usio wa Volti 12 (Chaja za simu, redio,…);
3. Vifaa vinavyotumia Volti 220 (TV, Friji) vinahitaji kirekibishi kingine kinachoitwa Inveta, kubadili Umeme wa DC kuwa AC.